KISWAHILI: Amani Wakati wa Uchaguzi na Msimamo wa Uislamu Kuhusu Uongozi

Uchaguzi ni tukio muhimu katika maisha ya kijamii na kisiasa ya taifa lolote. Ni kipindi ambacho raia hutumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi wa kuwawakilisha. Katika Uislamu, uongozi si heshima tu bali ni amanah (dhamana) kubwa ambayo kila mwenye akili timamu anatakiwa kuielewa kabla ya kuichukua au kuitekeleza.

Uislamu na Amani
Uislamu unasisitiza sana juu ya utulivu na amani, hasa wakati wa mitihani ya kijamii kama uchaguzi. Allah Subhanahu wa Ta’ala amesema:
"Na fanyeni suluhu baina ya ndugu zenu..." (Surah Al-Hujurat: 10)

Katika kipindi hiki nyeti, Waislamu wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa utulivu, busara, kujiepusha na lugha za chuki au uchochezi, na kushiriki uchaguzi kwa njia ya amani.

Kura ni Dhamana
Kuchagua kiongozi ni ibada inayohusiana na mustakabali wa jamii. Mtume (SAW) amesema:
"Kila mmoja wenu ni mchungaji, na kila mmoja wenu ataulizwa kuhusu alichokichunga." (Bukhari na Muslim)

Kwa hiyo, tunapaswa kuchagua viongozi wenye uadilifu, elimu, na khofu ya Allah – si kwa misingi ya ukabila, urafiki au maslahi binafsi.

Wito kwa Jamii

  • Tuendelee kudumisha amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

  • Tuwaelimishe wengine kuhusu wajibu wa kushiriki kwa njia sahihi.

  • Tuwakatae wazi wazi wachochezi wa fitna na vurugu.

  • Tumuombe Allah atupe viongozi waadilifu na wacha Mungu.


العربية: السلام وقت الانتخابات وموقف الإسلام من اختيار القادة

الانتخابات من الأحداث الهامة في حياة الأمم. وفي الإسلام، القيادة ليست تشريفاً فقط بل هي أمانة عظيمة يجب تحملها بوعي ومسؤولية.

الإسلام والسلام
يحث الإسلام على السلام والوفاق، خاصة في الأوقات الحساسة. قال الله تعالى:
{وأصلحوا بين أخويكم} [الحجرات: 10]

خلال الانتخابات، يجب على المسلمين أن يكونوا قدوة في ضبط النفس وتجنب الفتن، والمشاركة بطريقة سلمية.

التصويت أمانة
اختيار القادة مسؤولية كبيرة، وقد قال النبي صلى الله عليه وسلم:
"كلُّكم راعٍ، وكلُّكم مسؤولٌ عن رعيِته." (رواه البخاري ومسلم)

فلنختر من يخاف الله، العادل، المؤهل، وليس لأسباب قبلية أو شخصية.

دعوة للمجتمع

  • لنحافظ على السلام قبل وأثناء وبعد الانتخابات

  • لنتعلّم ونُعلِم غيرنا أهمية المشاركة السلمية

  • لنرفض دعاة الفتنة والعنف

  • ونسأل الله أن يرزقنا قادة صالحين يخافونه فينا


ENGLISH: Peace During Elections & Islam’s View on Leadership

Elections are vital moments in a nation’s political and social life. In Islam, leadership is not just a title – it is a trust (amanah) that carries great responsibility.

Islam and Peace
Islam strongly promotes peace and harmony, especially during sensitive times like elections. Allah says:
"Make peace between your brothers…" (Surah Al-Hujurat: 10)

Muslims must set an example by avoiding chaos, hateful speech, or violence, and participating in the process peacefully.

Voting is a Trust
Choosing a leader is a form of worship linked to the future of society. The Prophet (SAW) said:
"Each of you is a shepherd, and each of you is responsible for his flock." (Bukhari & Muslim)

Therefore, we should elect righteous, qualified leaders who fear Allah – not based on tribalism, friendship, or personal gain.

A Call to the Community

  • Maintain peace before, during, and after elections

  • Educate ourselves and others on proper civic conduct

  • Reject promoters of division and violence

  • Pray for pious and just leaders for our society

Comments